Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi.
Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika!
Nakupenda dear, amini moyoni umeniingia ndiyo maana mimba nikaamua kukubebea pasipo kunioa hakika mahaba yako yanifanya nijione malkia katika hii dunia! Nakupenda
Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.
Mhh kweli wewe ni mtaalam, unayejua kuitumia yako kalamu kila nikuonapo hupata hamu, hujihisi kupoteza fahamu, naomba ufahamu wewe ndio wangu mtaalam! Nakumiss
Kweli wewe ni mpishi! Umahiri wako unaanza kwenye ukunaji nazi hadi upakuaji. Upekechapo ndizi za mtori mimi huwa hoi. Nakupenda mpenzi.
Ooh My … . Hivi ni kweli umebanwa na kazi au unaniwekea pozi? Mawasaliano yalikuwa hayaishi tulipolianza letu penzi, leo si simu wala sms nizipatazo toka kwako mpenzi, hakika hunipendi siku hizi, enewei sina jinsi, zaidi ya kumshukuru mwenyezi!
Mmh! Nakumbuka siku ya kwanza maneno matamu uliyoniambia, ahadi kede ulinipatia, nakunifanya nijione malkia katika hii dunia, lakini leo umenibadilikia au kukupa penzi nimekosea?
Honey hivi unakumbuka? Ahadi uliyonipa, mwisho wa mwezi ukifika pesa utanipa, nitatuwe matatizo yaliyonifika, la azizi nakukumbusha tarehe zimefika, na tatizo langu bila wewe haliwezi tatulika! Luv u mwaah.
Mpenzi hakika ningekupa ila tarehe mbaya zimefika hali ya hewa imechafuka, vumilia wikiendi ijayo nitakupa, usiwe na pupa, mbivu zako nitakupa hakuna mwingine wakumpa, luv u.
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
Dhamira kuu ya Moyo wangu ni Mapenzi, kukupenda kwa dhati bila kipingamizi, kuishi nawewe kihalali kwa kudra za wazazi, Nipende nikupende Tudumishe Mapenzi. "NAKUTAKIA MCHANA MWEMA MPENZI WANGU"
Kwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa usoni, busu la amani hubusiwa mashavuni, busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la mapenzi hubusiwa shingoni, Je wapi nikubusu ili ulale kwa raha sweet ?
Naapa abadani penzi langu sitalitoa asilani ingawa upo mbali nami, nakupenda amini kwako nimefika, nitunzie langu penzi wasije niibia washenzi.
Hakikisho la mapenzi: . . umeingia moyoni mwangu kukutoa itakuwa ngumu sana,wajua moyo huwa unafunguliwa mara moja hasa kwa ile true love …
Leo ni zaidi ya mwezi toka tumeyaanza yetu mapenzi na kila kukicha nakuota kwenye njozi ukinipa majambozi na huishi uchokozi, sijui lini nitaacha hizi njozi kwa kunipa laivu lako penzi, nakupenda mpenzi
Sijui nini chakukukwambia furaha moyoni kila saa yanijia tangu ulivyoniambia mimba ndiyo ishaingia hivyo mtoto nikaye nikimtarajia, nakupenda dear hakika wewe pekee ndiye wangu malkia!
Naamini uatakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi, tafadhali badili yako mavazi , bafuni ingia upate maji kujimwagia, natamani kuja kukusaidia mgongo kuusugua na chakula kukuandalia lakini siku haijawadia, nakupenda dear