Thursday, 31 October 2019

SMS tamu za kimahaba

Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.


Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo,
ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi
yetu yadumu daima.
Nakupenda sana P tafadhari usinikasirikie, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu,
njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.


Nakupenda sana mwandani wangu ndiyo maana moyo wangu hupatwa kidonda ninaokuona na mwingine
hasa anapokuwa hana sifa, nahisi kama anakutumia wewe kama mdori wake wa kumfurahisha. Uwe makini ua la moyo wangu.
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia, fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu, fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo kwa kukutumia sms mpenzi wangu, Nakutakia usiku mwema
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali "NIACHE NIKUPENDE SWEET


Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee, lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"

No comments:

Post a Comment